BOFYA HAPO CHINI KUJIUNGA NA GRP LETU LA WAHSTAP

Uchovu mwingi pia unaweza kusababishwa na mtu mwenyewe. Ili wafikiemalengo yao na kupata pesa nyingi, baadhi ya watu hufanya kazi zaidi ya moja. Watu hao wana majukumu mengi na wanakabili hatari ya kuchoka kupita kiasi. Ikiwa unakabili tatizo la kuchoka kupita kiasi kazini, unawezaje kushinda tatizo hilo? Huenda ikaonekana vigumu kushinda tatizo hilo ikiwa kuna mambo yanayopita uwezo wako. Hata hivyo, chunguza hatua nne zifuatazo za kukabiliana na kuchoka kupita kiasi. Unaweza kupata suluhisho la tatizo lako
1. Chunguza Mambo Unayotanguliza
Ni nini muhimu zaidi kwako? Watu wengi wanasema kwamba uhusiano na familia zao na afya njema ndiyo mambo muhimu zaidi.Hivyo, ukichoka kupita kiasi familia yako itaathirikana afya yako itazorota.Ukizingatia mambo muhimu, itakuwa rahisi kwako kufanya maamuzi magumu na kukataa majukumu fulani. Kwa mfano, unaweza kugundua kwamba kazi yako inakusababishia uchovu unaopita kiasi. Hata hivyo, huenda ukasema, ‘Siwezi kubadili kazi au kupunguza muda ninaofanya kazi; ninahitaji pesa!’ Ni kweli, kila mtu anahitaji pesa, lakini kazi yako inaathirije mambo unayothamini zaidi? Uwe mwangalifu ili usitangulize mambo ambayo wengine wanaona kuwa muhimu. Huenda mambo ambayo ni muhimu kwa mwajiri wako yakatofautiana na mambo yaliyo muhimu kwako. Wengine wanaweza kutanguliza kazi kuliko mambo mengine maishani, lakini haimaanishi unapaswa kufanya hivyo.
2. Rahisisha Maisha Yako
Ili upunguze mkazo na upate muda wa kutimiza mambo unayothamini zaidi, huenda ukahitaji kufanya kazi kwa saa chache,kumwomba mwajiri wako akupunguzie majukumu,au ukahitaji kubadili kazi. Vyovyote vile, inaelekea utahitaji kupunguza matumizi ya fedha na kubadili mtindo wako wa maisha. Inawezekana kufanya marekebisho hayo, na huenda isiwe vigumu kama unavyowazia.Katika nchi nyingi, wafanyabiashara wanashawishi watu wanunue bidhaa, na wengi wanafikiri kwamba furaha inatokana na kupata utajiri. Hata hivyo, si kweli. Maisha rahisi yanaweza kukuletea uhuru mwingi na kufanya uridhike. Ili ufanikiwe kufanya mabadiliko hayo, unahitaji kupunguza matumizi yako na kuweka akiba ya pesa. Jitahidi kupunguza au kuepuka madeni. Zungumza na familia yako kuhusu umuhimu wa mabadiliko hayo na uwaombe wakuunge mkono.
3.Jifunze kukataa Kazi
kazi nyingine,ni rahisi kupata kazi nyingine ukiwa bado kazini.Hata kama mwajiri wako atakubali ufanye kazi kidogo ujue kwamba huenda baadaye akasisitiza ufanye kazi zaidi. Ni nini kitakachokusaidia kudumisha msimamo wako? Jitahidi kudumisha makubaliano yenu ya awali.Kufanya hivyo kutakupa uhuru wa kumwomba mwajiri aendelee kufuata makubaliano hayo.
4.Uwe na Muda wa Kupumzika
Hata ukifaulu kupunguza kazi, huenda bado utapatwa na mkazo, utashughulika na watu wagumu, au hali zisizopendeza. Uwe na muda wa kupumzika vya kutosha na uwe na burudani kwa kiasi. Kumbuka kwamba si lazima utumie pesa nyingi ili ufurahie burudani pamoja na familia yako.Mbali na kazi, uwe na mambo unayofurahia kufanya na pia uwe na marafiki, na uepuke kufikiria kazi tu kila wakati. Kwa nini?Kitabu Your Money or Your Life kinasema hivi: “Utu wako ni muhimu kuliko kazi unayofanya ili kupata pesa.” Ikiwa unafikiri utambulisho wako au heshima yako inategemea kazi yako, huenda ukashindwa kuweka mpaka kati ya kazi na shughuli zako mwenyewe.
Credits to JW journal
ILI UWEZE KUANGALIA VIDEO YAKE GUSA HAPA CHINIII
Post a Comment